Viongozi wa TaTEDO SESO wamtembelea Mheshimiwa Spika Bungeni Dodoma

  • Category: Events
  • Published: Thursday, 04 May 2023 09:49
  • Written by Webmaster
  • Hits: 912

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya TaTEDO SESO ambao ni watengenezaji na wasambazaji wa bidhaa za nishati safi zinazotumia umeme kwa gharama nafuu.

Kikao hicho kimefanyika Aprili 19, 2023 Ofisini kwake Bungeni, Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi Mtendaji wa TaTEDO SESO, ndugu Estomih Sawe amemuelezea na kumuonyesha Mhe.Spika jiko sanifu la umeme lenye presha, linalotumia umeme kidogo, linalookoa muda, fedha linatunza mazingira na kuondokana na ukataji wa miti, na linatunza virutubisho, halisababishi joto jikoni, haliunguzi chakula, jiko hilo (julep) linatumika kupikia vyakula vyote vya Kitanzania. Amewaasa Watanzania wote kutumia jiko hilo bora la umeme.

Viongozi wa TaTEDO SESO wamtembelea Mheshimiwa Spika Bungeni Dodoma      Viongozi wa TaTEDO SESO wamtembelea Mheshimiwa Spika Bungeni Dodoma





2022 © Tatedo - Sustainable Energy Services Organization. All Rights Reserved. Designed by microsafi.com