Fahamu jinsi ya kujikinga na virusi vya corona

  • Category: News
  • Published: Saturday, 04 April 2020 05:21
  • Written by Webmaster
  • Hits: 782

Watu wengi huvaa vinyago kote duniani kwa kujikinga na ugonjwa wa corona. Lakini hatua nyingine ni muhimu zaidi.Ufuatao ni muelekezo wa shrika la afya ulimwenguni WHO kwa kujikinga na virusi vya Corona.

Bora kuliko kukosa

Haija thibitishwa ikiwa vinyago vya kuvaa usoni/mask vinaweza kumkinga mtu na kutoambukizwa virusi vya Corona.Lakini vinyago hivyo vinaweza kuzuwiya baadhi ya vijidudu kabla havija gusa kinywa na pua .Na ikiwa una ugonjwa tayari, kinyago hicho kitazuwiya kutoambukiza wengine.

Osha mikono na sabuni

Kwenye daftari lake la maelekezo katika kupambana na Corona, shirika la afya ulimwenguni WHO halijaorodhesha kuvaa kwa vinyago vya uso. Hatua ya kwanza ni kuosha mikono. WHO imependekeza kutumia maji yenye mvinyo kama inavyoonekana kwenye picha.

Sabuni na maji hutumiwa pia

Suluhisho la kila siku ni kuosha mikono kwa maji na sabuni, lakini hakikisha kwamba umeisafisha vizuri.

Kukohoa na kuchemua lakini ufanye kwa maelekeo mazuri.

Yafuatayo ni maelekezo ya madaktari : Unapokohoa na kuchemua zuwiya kinywa na pua yako au tumia kitambaa cha kujifutia na baadae kukitupa na kuosha mikono.

Baki kando!

Mwelekezo mwingine ni kutoenda kwenye maeneo ya watu wengi au kuwa karibu na mtu alie na homa au mafua na ikiwa hivyo hakikisha kwamba umechukuwa hatua bora za kiafya.

Una homa? Nenda kwa daktari na usisafiri!

Ikiwa una homa, kikohozi, na una matatizo ya kupumua ,ni lazima kuomba huduma za kiafya haraka iwezekanavyo. Epuka maeneo ya watu wengi ili usije kuwaambukiza wengine. Umpe maelezo daktari kuhusu maeneo ulioyatembelea

Epuka misongamano!

Unapokwenda kwenye maeneo ambako virusi vya corona vimeripotiwa, epuka kukaribiana na wanyama walio hai na maeneo yaliofikiwa na wanyama hao.

Mapishi bora!

Pika chakula vizuri hasa nyama, epuka matumizi ya nyama mbichi au isiyopikwa vizuri. Nyama mbichi, maziwa na viungo vya wanyama vinatakiwa kutumiwa vizuri. Maelekezo hayo yanasaidia kuepuka maambukizi ya virusi hivyo.





2022 © Tatedo - Sustainable Energy Services Organization. All Rights Reserved. Designed by microsafi.com