TAASISI ISIYO YA KISERIKALI TATEDO YAENDELEA KUFANYA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI
- Category: News
- Published: Thursday, 10 March 2022 12:31
- Written by Webmaster
- Hits: 751
Taasisi isiyo ya Kiserikali Ya kuendeleza Nishati Endelevu na Uhifadhi ya Mazingira TATEDO inaendela Kutoa Mafunzo kwa vikundi vya Wajasilia mali wadogo wilayani kisarawe mkoani Pwani wakiwa na Lengo la kuweza kuwapa elimu ili waweze kujikwamua ki uchumi.
Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mhandisi, Hanan Mohamed, Afisa Maendeleo ya wilaya ya kisarawe Salma Rasuli Ambaye pia alitoa Mafunzo hayo alisema.
Mafunzo hayo yana umhimu kwa wajasiliamali ili kuwajengea uwezo wa kutambua ni namna gani waweze kukuza biashara zao, pia aliwataka wanavikundi mbalimbali vya biashara waweze kujitokeza kwenye matamasha mbalimbali ili waweze kujifunza vitu vipya