Ecook Book (Kiswahili)
- Category: E-cook manuals
- Published: Thursday, 27 August 2020 08:07
- Written by Webmaster
- Hits: 595
Mwongozo huu wa kupika kwa kutumia umeme unalenga kuongezauelewa kuhusu masuala ya majiko, vifaa na nishati za kisasa za kupikia,hususani kupika kwa kutumia nishati ya umeme. Katika kufikia lengo lakutoka kutumia nishati za kuni na mkaa na kutumia nishati safi, za kisasana endelevu kupikia, tunawaletea suluhisho sahihi na endelevu ambaloni Jiko Sanifu la Umeme Lenye Presha ( JULEP).
Katika mwongozo huu, tutajifunza mambo mbalimbali yanayohusu kupikakwa kutumia umeme, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kutumia JULEP kwamapishi mbalimbali ya kitanzania. Pia tutaona jinsi ambavyo jiko hili lenyeufanisi mkubwa linavyoweza kuokoa fedha, nishati, afya na misitu yetu.Pia mwongozo huu unatoa majibu ya changamoto mbalimbali kuhusumasuala yanayohusu kupika kwa kutumia umeme, upatikanaji wa majikoya JULEP na hamasa yake ndogo.