Firewood Stove Manual
- Category: E-cook manuals
- Published: Sunday, 31 May 2020 11:41
- Written by Webmaster
- Hits: 693
UTANGULIZI1
Hali ya Nishati ya Tungamotaka TanzaniaNishati ni mojawapo ya mahitaji muhimu kwa maendeleo ya kaya, jamiina taifa kwa ujumla. Zaidi ya asilimia 80 ya nishati yote inayotumikanchini Tanzania hutokana na tungamotaka (hasa kuni na mkaa). Takwimukutoka vyanzo mbalimbali zinaonesha kuwa watumiaji wakubwa wanishati ya tungamotaka ni kaya, taasisi (shule, magereza, n.k) na wenyebiashara ndogo na za kati (migahawa, wakaanga samaki, n.k). Tungamotakani chanzo kikubwa cha nishati ya kupikia kwa zaidi ya asilimia 92 yawatanzania wote. Misitu ya jamii na hifadhi ni chanzo kikuu cha kunina mkaa. Takwimu zinaonesha kuwa mahitaji ya nishati ya tungamotakayanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na kukosekana kwa nishatimbadala ambayo jamii inamudu gharama zake. Kuongezeka kwa mahitaji yatungamotaka kumepelekea uharibifu wa misitu na kuleta madhara ya kiafyakwa watumiaji. Mwaka 2015 Tanzania inakadiriwa kupoteza takriban ekari372,816 za misitu kwa mwaka, takwimu za hivi karibuni 2018 zinaoneshaupotevu umeongezeka kufikia ekari 469,420 kwa mwaka.