Baking Manual - Swahil
- Category: E-cook manuals
- Published: Sunday, 31 May 2020 11:45
- Written by Webmaster
- Hits: 732
Malengo ya MwongozoUokaji unatoa fursa ya kibiashara kwa wananchi kujiongezea kipato na ajirahasa kwa makundi ya akina mama na vijana. Uokaji wa kawaida umekuwaukitumia kiasi kikubwa cha nishati ya mkaa na kuongeza gharama ya uokaji.Kwa kuitambua changamoto hiyo, TaTEDO ilibuni na kutengeneza maovenisanifu yanayotumia mkaa kuokea aina mbalimbali za vyakula.Pamoja na kuwa kuna aina mbalimbali za oveni zinazopatikana TaTEDO,mwongozo huu unaelezea aina ya oveni ijulikanayo kama Oveni Kabati.
Oveniya aina hii hutumika zaidi kuokea mikate, skonzi, keki na “cookies”. Uokajikwa kutumia oveni hii huhitaji mtumiaji kuwa na uelewa wa kutosha kuhusujinsi ya kuitumia. Mwongozo huu umetayarishwa ili kusaidia watumiajiwa oveni ya aina hii kupata uelewa jinsi ya kuitumia, mambo ya msingi yakuzingatia katika uokaji na fursa za kibiashara zilizopo katika uokaji.