Katalogi ya teknolojia za nishati endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Tanzania, Afrika Mashariki
- Category: INFORSE latest
- Published: Tuesday, 11 April 2023 12:05
- Written by Webmaster
- Hits: 766
Kipeperushi hiki kinatoa muhtasari wa Katalogi ya teknolojia zipatazo 80 za nishati endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi zinazopatikana Afrika Mashariki hususani nchi ya Kenya, Uganda, na Tanzania. Katalogi hiyo inapatikana kwa njia ya mtandao na pia kwenye chapisho lenye kurasa 150.
Toleo la mtandaoni linatoa fursa ya kufanyiwa maboresho ya mara kwa mara na wadau wanakaribishwa kuchangia kuiboresha kwa kuingiza teknolojia mpya.
Madhumuni ya Katalogi ni kutoa uelewa juu ya upatikanaji na mchango wa teknolojia za nishati endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kutatua changamoto zilizoko ndani ya jamii.